New life in Christ

New life in Christ (Maisha mapya ndani ya Kristo) zamani ikijulikana kama (New Life Crusade), ni huduma ya kikristo inayowaunganisha Wakristo toka madhehebu mbalimbali hapa Tanzania waliompokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Huduma hii ipo karibu mikoa yote ya Tanzania na inatokana na Uamsho wa Africa ya Mashariki ulioanzia Rwanda, Uganda, Kenya na kasha Tanzania mara baada ya vita ya kwanza ya dunia. 1917 .Mwaka 1963 August ulifanyika mkutano mkubwa wa injili hapo hapa Dar-es-Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo marehemu Askofu Yohana Omari wa dayosisi ya Kiangilikana ya Morogoro alihubiri. Kutokana na umuhimu uliojitokeza wa kuwalea waliookolewa ktk mikutano hii pasipo kuanzishwa kwa dhehebu jipya au kuwahamisha toka katika madhehebu yao na kutunza mali na fedha zilizotokana na uinjilist huu, huduma ya New Life Crusade na hatimaye New life in Christ (N.L.C) ilianzishwa. N.L.C ilisajiliwa rasmi serikalini tarehe 30/ 04/ 1990. Tangu kuanzishwa kwake mpaka sasa, Read more